JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mkazi
wa kitongoji cha Mihuru, kijiji cha Kitarungu wilayani Serengeti, Mara
amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni
kukosa ng’ombe wa kulipa mahari.
Chacha Bruna (25) alijinyonga kati ya Septemba 7 na 8 usiku baada ya kunyaang’anywa mke kwa kukosa mahari hiyo ya ng’ombe.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Yohana Gimano alisema Bruna alifikia uamzi huo baada ya
kunyang’anywa mwanamke kwa kushindwa kulipa mahari.
“Yeye
ni mkazi wa Tarime lakini hapa kijijini kuna ukoo wao, alipofika hapa
alimtorosha binti mmoja (Rhobi Samweli) akakaa naye kwa muda wa siku
nne. Septemba 7 ndugu zake walimfuata huyo binti ili atoe mahari,
akaambiwa atoe ng’ombe tisa, yeye akasema anaye mmoja, wakamfukuza mpaka
atoe mahari ndipo apewe mke, usiku akaamua kujiua,” alisema.
Alisema
kuwa kabla ya kuchukua uamzi huo akiwa na kamba ya katani alimwambia
mwanamke mmoja kwenye mji aliokuwa anaishi kuwa haoni faida ya kuishi na
kuwa siku hiyo ndiyo mwisho wake. Hata hivyo, hawakufuatilia kwa kuwa
hawakutegemea kama angechukua uamzi huo.
“Asubuhi
walikuta ananing’inia kwenye mti pembeni ya barabara akiwa ameshakufa.
Inaonekana alijinyonga usiku ule ule kwa kuwa wanadai hata chakula cha
usiku hawakula naye, walijua yuko katika matembezi ya kawaida,”
alibainisha.
Mwalimu
mkuu wa shule ya Msingi Kitarungu, Emmanuel Matiko ambaye ni jirani
yake alisema waliugundua mwili huo asubuhi baada ya wanafunzi waliokuwa
wakienda shule kuukuta mwili wake ukining’inia.
“Suala
la yeye kunyang’anywa mwanamke linajulikana na alionekana mwenye mawazo
sana baada ya kushindwa kuelewana na ndugu wa mchumba wake. Huenda
ilimuathiri kisaikolojia na kukosa msaada wa ushauri,” alisema.
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz



Post a Comment