JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Sept 18, Mwanasheria
wa CHADEMA ambaye ni mkuu wa idara ya Uchaguzi kwenye sheria,Bw.John
Mallya alifanya mkutano wa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu uki
ukwaji wa sheria na chama pinzani.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari..’Ndugu
waandishi wa habari tumewaita hapa hususani mambo ya kisheria
yanayoendelea kwenye kampeni zoezi la uchaguzi ni zoezi la kikatiba,
sheria ya uchaguzi wa taifa mwaka 1985 kanuni za uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 na maadili ya uchaguzi wa Ubunge, Urais na Udiwani pamoja na sheria
nyingine ikiwemo ya rushwa na sheria ya vyama vya kisiasa – John Mallya
‘Sheria kwa mfano ambayo ni maadili ya
Uchaguzi ya mwaka huu vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu kupitia
makatibu wake wakuu wameweka sign zao inakataza kwa mfano suala la mtu
kutoa bango la mtu mwingine lakini chadema imepata hiyo changamoto
kwamba mabango yake wameondolewa kwa mfano hili bango lipo Nyerere Road
pale Mwanza limeondolewa na watu wa CCM ilikuwa ni nyumbani ya mtu
binafsi wakamtishia watachoma nyumbani yake wakamrushia mawe wakavunja
vioo vyake na baada wakaliondoa‘ – John Mallya
‘Na hii inaonesha sio tu ni namna gani
CCM sio tu wamekiuka sheria lakini hawafai kutawala nchi kwasababu
suala la kuweka bango ni suala la kisheria ukiona bango la
Samia,Magufuli na mtu yoyote limewekwa kisheria‘ – John Mallya
‘Mabango, sera, vipeperushi vyote vinakuwa vimesajili na tume ya Uchaguzi kwa madhumuni ya Kampeni kwa mfano
ujumbe wa Mabadiliko umesajiliwa na nembo ya CHADEMA pia imesajiliwa,
sasa CCM wanakiuka sheria wame ku copy na ku paste wanachukua ilani na
sera zetu ambapo wamechukua nembo yetu M4C ambayo sisi tunaita Movement 4
Change huku CCM wakiwa wanasema M4C ni Magufuli 4 Change‘ – John Mallya
‘Katika hili tumechukua hatua nzito
kuliko hizi za mwanza maana yake hili sio la kimadili hili ni uvunjwaji
wa sheria, Chadema tunampeleka Magufuli Mahakamani pamoja na bodi ya
wadhamini wa chama cha Mapinduzi‘ – John Mallya
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz






Post a Comment