JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Wananchi
wilayani kahama mkoani shinyanga wameombwa kuwa makini katika kipindi hiki cha
kampeni za uchaguzi mkuu wa madiwani
wabunge na rais ili kuchagua viongozi
watakaoleta maendeleo katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa
leo mjini kahama na mgombea wa kiti cha
urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli katika mkutano wa
kampeni zake uliofanyika katika viwanja vya milango kumi mjini humo.
Magufuli amesema
katika kipindi hiki cha kampeni baadhi
ya wagombea wanatumia sera nyingi za udanganyifu kwa wananchi wao na ambazo
kamwe hawawezi kuzitekeleza, hivyo kuwataka wananchi kutowachagua.
Magufuli amesema
watanzania wamekuwa wakipotoshwa kuwa chama kilichopo madarakani hakijaleta
maendeleo kwa watanzania bila kutazama maendeleo ya miundo mbinu kama barabara,
maji na shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizojengwa na chama cha mapinduzi.
Ameongeza kuwa
ndani ya CCM kuna baadhi ya viongozi ambao sio waadilifu wanaokichafua chama
hicho, hivyo ameahidi kuleta mabadiliko katika chama hicho na maendeleo kwa
wananchi huku akisisitiza kulinda umoja na amani ya nchi.
Mkoa wa
shinyanga ni mkoa wa 15 kati ya mikoa ambayo Magufuli amefanya kampeni zake
tangu kampeni hizo zilipozinduliwa, ambapo awali kabla ya kufika mjini kahama amefanya kampeni
katika jimbo la Ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz



Post a Comment