Loading...

Tope linapotumika kama tiba ya ngozi

> JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HAPA CHINI UPATE NAFASI..

JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..

Mwanamke akiwa amekandikwa tope kama sehemu ya tiba.

TOPE lenye tiba limekuwa likichimbwa katika ghuba ya Haapsalu na kutumika kwa mafanikio tangu mwanzoni mwa karne ya 19. 

Tafiti za mwanzo za tiba hiyo imeanza katika kipindi hicho.


Kwa takribani miaka 200, matumizi ya jadi ya tope lenye tiba yamechangia kuwepo tiba ya magonjwa mbalimbali. Tope hilo linatajwa kuponya magojwa sugu ya ngozi, magonjwa ya uzazi, kuondoa sumu mwilini, kutibu maumivu ya miguu na viungo vingine vya mwili, gauti na uchovu.

Mkuu wa taasisi ya Fra Mare Thalasso Spa, Maret Suckles anasema, tiba ya tope linalopatikana katika Bahari ya Baltic imekuwa likitumika kutibu watu wenye magonjwa kutoka ndani na nje ya Estonia.

Suckles anasema, baada ya tope hilo kuchimbwa kwenye kina cha bahari kwa mitambo inayowekwa kwenye boti ndogo, hufikishwa katika kituo cha afya kupitika bomba na kupelekwa eneo la kuhifadhiwa.

“Kiasi cha kati ya tani 42 hadi 72 huchimbwa na kutumika kila mwaka, na kiasi hicho kinategemea idadi ya wagonjwa wanaotarajiwa kupata tiba hiyo katika kipindi husika,”anasema Suckles.

Anasema tiba ya mgonjwa inatokana na maelekezo ya madaktari katika hospitali hiyo wanaotoa maelekezo ya tiba kulingana na tatizo la mgonjwa. 

Kwa mujibu wa Suckles, kuna wagonjwa wanaopakwa dawa hiyo mara moja na matatizo yao yanakwisha lakini wengine huchukua muda mrefu na kutakiwa kurudi tena hospitalini kuendelea na dozi nyingine kulingana na aina na ukubwa wa tatizo la mgonjwa.

Anasema tiba hiyo imefanyiwa utafiti wa kina na kwamba inatokana na aina ya madini adimu yanayopatikana katika Bahari ya Baltic. 

Kiongozi huyo anasema, baada ya tope kufikishwa katika hospitali hiyo, hutengwa kiasi cha kutosha kwa wagonjwa watakaohudumiwa kwa siku husika na kuchemshwa hadi kufikia nyuzi joto kati ya 38 hadi 42, na kisha humpaka mgonjwa kulingana na maelekezo ya daktari.

“ Mtu huwekwa ndani ya beseni maalumu akiwa amepakwa tope mwili nzima, hapo unakuwa kama upo ndani ya sauna (bafu la joto) na utatakiwa kubaki na tope hilo lenye joto ndani ya dakika 15 hadi 20 kulingana na tatizo lako na kisha kuondolewa,” anasema Suckles.

“Robo saa tu baada ya kuanza tiba ya tope, mgonjwa hutoka jasho, mzunguko wa damu unabadilika, ngozi inaanza kuuma hiyo kuonyesha kuwa tope linafanya kazi. “ Misuli iliyosinyaa huamshwa kwa tiba hii, huchangamsha mzunguko wa damu, hunyonya majimaji yaliyozidi mwilini na inaondoa maumivu.

Wakati wa tiba hii, mgonjwa hufunikwa kwa blangeti au mifuko mikubwa ya plastiki ili kulinda joto la tope lisipotee haraka kabla tiba kukamilika hasa kutokana na nchi yenyewe kuwa ya baridi. Anasema, mgonjwa anayehitaji tiba hiyo hutakiwa kulipa kiasi cha euro 300 (sawa na Sh 720,000) kwa tiba ya wiki moja.

Gharama hiyo inajumuisha huduma za kifungua kinywa, chakula cha mchana na usiku, mazoezi ya kutembea, mazoezi kwenye gym, mazoezi ya viungo kwenye bwawa la kuogelea na huduma ya bafu la joto (sauna).

‘Mara nyingi wagonjwa hupewa tiba kwa wiki moja au zaidi kulingana na aina ya ugonjwa, hivyo gharama hizo pia hujumuisha gharama za malazi na gharama za kumuona daktari ambaye anatakiwa kuwaangalia wagonjwa wake kwa saa 24,” anasema.

Katika jumba la Fra Mare, wagonjwa wengi wanaonekana ni wazee, wake kwa waume ambao kila mmoja anakuja na tatizo lake. Suckles anasema, wagonjwa wengi wanaofika kupata tiba ni wageni kutoka nchi za Ulaya ikiwemo Sweden, Finland na Urusi.

“ Hakuna wagonjwa wanaotoka Afrika moja kwa moja, ila tumekuwa tunawapokea Waafrika ambao wanaishi katika nchi mbalimbali za Umoja wa Ulaya ( EU),” anasema. Kwa mujibu wa Suckle, kutokana na tiba hiyo, kwa mwaka kituo cha Fra Mare kinakusanya faida ya takribani euro milioni mbili ambazo ni sawa na bilioni 4.8.

Suckle anasema pamoja na uzuri wa tiba hiyo, kuna masharti ya kufuatwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya uvimbe, kifua kikuu, ujauzito, figo, magonjwa ya akili, bawasiri na homa. “Watu wenye matatizo haya wanahitaji kupewa ushauri na daktari kabla ya kuanza kutumia tiba ya tope,” anasema.

Mmoja wa wagonjwa kutoka Finland, Marut Garlaal (74) anasema, amefika katika kituo cha afya ili kupata tiba ya miguu ambayo imekuwa ikimsumbua kwa maumivu kwa muda mrefu. “Nasumbuliwa sana na maumivu ya miguu, nadhani tatizo langu linatokana na utu uzima.

Nimeambiwa tiba hii itanisaidia, sijali kama ni tope au ni nini, lakini nataka kupona,” anasema Garlaal. “Nimeshaanza matibabu, na ni vigumu kukaa na tope mwilini hata kwa sekunde tatu kutokana na harufu na joto lake, lakini kwa kuwa ni tiba inayoaminika sina budi kuvumilia na kuitumia,” anasema.

Magonjwa mengine yanayotibiwa na tope hilo, ni pamoja na kidonda baada ya kufanyiwa upasuaji, maumivu ya mgongo, mishipa ya fahamu, misuli, kipanda uso, magonjwa ya koo na sikio sugu.

Mwaka 1825, Mjerumani Dk Carl Abraham Hunnius alikuwa ni mtu wa kwanza kubaini tiba hiyo baada ya kuwaoana wenyeji wa mji huo wakitumia tope la Bahari ya Baltic kutibu maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua.

Hali hiyo inamshawishi kuanza kulifanyia uchunguzi tope hilo kwa kujenga bafu la matope alilolijenga katika mji wa Haapsalu. Baada ya hapo mfalme Czar Peter wa kwanza, Alexander wa kwanza na wa pili walikuwa ni miongoni mwa viongozi waliofika Haapsalu wakitoka mji wa Petersburg kwa lengo la kuimarisha afya zao kwa kutumia tope.

Mwaka 1958 baada ya mlipuko wa ugonjwa wa polio, Profesa Ernest Raudam kutoka Chuo Kikuu cha Tartu, Estonia alifungua hospitali ya kutibu ugonjwa huo kwa njia ya tope ili kuwapa tiba waliopooza. Tope hilo lina kemikali kadhaa zinazotokana na udongo na mazao ya bahari na madini ya bahari ikiwemo chumvi, salfa na oganiki. >
JISHINDIE SAMSUNG GALAXY MPYA KABISA JAZA FOMU NA UTAPIGIWA SIMU PAPO HAPO BOFYA HAPO JUU,RUDIA KUBOFYA MPAKA UONE SIMU UNAPIGIWA =>

Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by Lovetzz

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WANAWAKE KWANZA | Modified By Zotekali WEB Exparts
Back To Top