JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mwanaume mmoja
20,aliyetumia Facebook kumtongoza mwanafunzi mwenza kwa nia ya kushiriki
ngono naye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela nchini Marekani.
Owen
Labrie alipatikana na hatia ya kumtongoza msichana huyo ambaye jina
lake limebanwa kwa sababu ya umri wake mdogo wa miaka 15.
Labrie na msichana huyo walikuwa wanafunzi wa shule moja ya kifahari sana mjini Concord, New Hampshire.
Wakati
wa kusikizwa kwa kesi hiyo, wakili wa mshtakiwa alidai kuwa ni desturi
ya wanafunzi wanaokamilisha masomo kuwaalika wanafunzi wapya shuleni
humo kisha wakashiriki ngono nao katika tamaduni inayojulikana kwa jina
la uzushi ''kupiga saluti''
Shule hiyo ya kifahari na ghali ya St
Paul inajivunia kuwa kitovu cha elmu kwa mamia ya viongozi wa kada
mbalimbali nchini Marekani akiwemo waziri wa maswala ya kigeni John
Kerry.
Wanafunzi wengine waliosomea katika shule hiyo ya ''Kupiga saluti'' ni mabalozi 13 na watafiti wenye hadhi ya juu duniani.
Katika kujitetea wakili wa Labrie aliomba mahakama imhurumie
mteja wake kwani huo ulikuwa ujinga wa matineja waliokuwa mbioni
wakitaka kukubalika na wenzao.
Jaji wa mahakama ya juu Larry Smukler alimtaja Labrie kuwa 'muongo wa kupindukia' alipotoa hukumu hiyo ya mwaka mmoja gerezani.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz



Post a Comment