JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida watu 5 kati ya 6 waliyokuwa wamefunikwa na
kifusi kwa siku 41 katika machimbo madogo wa nyangalata wilayani kahama
mkoani shinyanga wameokolewa wakiwa hai.
Wakizungumza
leo na kahama fm wakati wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa
kahama, wahanga hao wamesema hali hiyo imewakuta katika harakati za
kuwaokoa wenzao waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika machimbo hayo.
Wahanga
hao ni Onyiwa Kanyimbo(55),Msafiri Jerald(38) Amosi Muhangwa(25),
Chacha wambura(53) na Joseph Burule(44) na aliyefariki dunia ni Mussa
Supana.
Wamesema
walikuwa wakiishi kwa kunywa maji, na kula magome ya miti pamoja na
mende hali iliyowasababisha kuendelea kuwa hai kwa siku 41 hadi jana
jioni walipookolewa.
Menaja
wa mgodi mdogo huo Amosi Mbanga amesema timu ya mafundi ilifanya
utafiti na kugundua kuna sauti za watu zikiita na kuamua kupeleka
uwokawaji kushirikiana na serikali pamoja kampuni acaica na kufanya
uokowaji huo ulichukua masaa 24.
Naye
kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kahama Dk. Jibai Mkama
amethibitisha kuwapokea wahanga hao na kwa sasa hali zao zinaendelea
vizuri wakiwa bado wanapatiwa matibabu katika hosspitali hiyo.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz




Post a Comment