JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Farasi huweza kubaini kati ya mtu aliye na furaha na aliye kasirika kwa kuangalia uso wa mwanadumu,utafiti umesema.
Katika jaribio, kwa kutumia picha za mwanamume wanasayansi
kutoka chuo kikuu cha Sussex walionyesha kwamba farasi wanaofugwa
nyumbani huchukizwa na sura zilizokasirika.
Wanasayansi hao wanasema kuwa ufugaji huo huenda umewawezesha farasi kuelewa tabia za binaadamu.
Matokeo hayo yamechapishwa katika jarida la Biology Letters.
Kundi hilo lilifanya vipimo vyake kwa kuwasilisha picha nyingi mbele ya farasi 28.
''Mtu mmoja anashikilia farasi huku mwengine akishikilia picha,''alielezea mtafiti Amy Smith.
Matokeo yake ,alielezea ni kwamba waliangalia picha za watu waliokasirika na jicho lao la kushoto.
Akili
za wanyama zimeumbwa kana kwamba hisia zinazotolewa na jicho la kushoto
huangaziwa na eneo la kulia la ubongo ambalo hutumiwa kuangazia hisia
mbaya.
Watafiti hao pia waliweka vipimo vya moyo katika moyo wa
farasi hao ,ambavyo vilibaini kwamba nyuso zilizokasirika hufanya myoyo
ya wanyama hao kudunda kwa haraka.
Matokeo kama hayo yameripotiwa
miongoni mwa mbwa na kuzua maswali kuhusu ni vipi kuishi na binaadamu
kuna badili tabia za wanyama hao.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz



Post a Comment