JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje (pichani)
anakusudia kuita mahakamani zaidi ya mashahidi 693 kupinga ushindi wa
mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula (CCM).
Wakili
wa Wenje, Deya Outa aliieleza mahakama kuwa mashahidi hao ni pamoja na
waliokuwa wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, wakati wa
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
“Tunatarajia
kuita mahakamani mashahidi wasiopungua 693 kuthibitisha madai yetu,
kulingana na mahitaji ya hoja tunazotaka kuzithibitisha mahakamani,” alidai wakili Outa.
Pande
zinazohusika kwenye shauri hilo namba 3 la mwaka 2015, juzi ziliweka
wazi hoja wanazokubaliana na zile wanazobishania kabla ya Jaji Mfawidhi
wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo anayesikiliza shauri
hilo kuihairisha hadi Machi 14, mwaka huu, itakapoanza kusikilizwa
mfululizo.
Pamoja
na Mabula, wadaiwa wengine katika shauri hilo linalovuta umati wa
wasikilizaji ni aliyekuwa msimamiza wa uchaguzi Nyamagana na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.
Kutokana
na wingi wa mashahidi na muda wa mwaka mmoja uliowekwa kisheria wa
mashauri ya uchaguzi kusikilizwa na kuamuliwa, wakili Outa alisema iwapo
muda huo utaisha kabla hawajamaliza kutoa ushahidi wao, wataiomba
mahakama kuwaongezea muda wa ziada.
Lembeli apeta
Aliyekuwa
mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini kupitia Chadema, James Lembeli
ameruka kihunzi kingine baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Shinyanga inayosikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo
hilo kutupilia mbali pingamizi la mashahidi wa mlalamikaji lililokuwa
limewekwa na mawakili wa upande wa mshitakiwa.
Akitoa
uamuzi huo jana mjini Kahama, Jaji Moses Mzuna alisema ni kinyume cha
sheria na wala siyo haki kuzuia mashahidi wa mlalamikaji kutoa ushahidi
wao, hivyo ni vyema wakatoa na haki ikatendeka.
Uamuzi
huo ulifuatia mvutano mkali wa kisheria uliotokea Machi 4, mwaka huu,
baina ya mawakili wa upande wa utetezi na wakili wa mlalamikaji ambapo
Jaji Mzuna aliahirisha shauri hilo, hadi alipolitolea uamuzi jana
asubuhi.
Katika
mvutano huo, mawakili wa utetezi Anthony Nasimire, Denis Kahangwa na
Castuce Ndamugoba walipinga mashahidi wa Lembeli kutoa ushahidi wao
kwakuwa walikiuka sheria inayowataka kuwasilisha viapo vyao mahakamani
ndani ya saa 48, kabla ya shauri kuanza kusikilizwa.
Pia
Jaji Mzuna alisema sheria hiyo ni mpya na kwamba haikujulikana kwake,
kwa mawakili wa pande zote, na hata katika rejea za kimahakama nchini
ndiyo maana hata mawakili wa utetezi wameiwasilisha wakati ushahidi
umekwishaanza kutolewa.
Alifafanua
kwamba sheria ya uchaguzi inaelekeza mlalamikaji kutoa ushahidi
usioacha mianya ya mashaka, jambo ambalo pia mahakama iliona si vyema
mashahidi walioandaliwa kuzuiliwa kutoa maelezo yao, hali itakayobana
uwigo wa upatikanaji wa haki.
Kwa
upande mwingine Jaji Mzuna aliikataa hoja ya wakili wa Lembeli, Mpale
Mpoki kwamba muda wa kuandaa viapo haukuwepo kwa kuwa ilimchukua muda
mwingi kuandaa shauri hilo, ambapo Jaji Mzuna alisema haikubaliki
kisheria.
Hata
hivyo alisema kuchelewa kwa Mpoki kupeleka viapo vya mashahidi hakuwezi
kuwa sababu ya Lembeli kupoteza fursa ya kudai haki yake anayohisi
alipokonywa, bali muda zaidi umetolewa wa kuandaa viapo hivyo.
Kufuatia
hali hiyo Jaji Mzuna aliahirisha shauri hilo hadi Machi 15 mwaka huu
ambapo mahakama itaanza kusikiliza maelezo ya mashahidi wa Lembeli
waliokuwa wamesubiri uamuzi dhidi ya mvutano huo wa kisheria uliopinga
mbunge huyo wa zamani wa jimbo la kahama asipeleke mashahidi wake
mahakamani.
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz


Post a Comment