JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..

Katika
hali isiyokuwa ya kawaida watu watano wamefariki dunia papo hapo kwa
kukatwa katwa mapanga kama wanyama katika kitongoji cha Kisesa kata ya
Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
Watu
hao ambao ni wa familia moja walifanyiwa unyama huo kwa kukatwa katwa
mapanga sehemu ya shingoni, huku wahusika wa tukio hilo wakiwa
hawajajulikana.
Akitoa
taarifa mbele za waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa
Gemine Mushy alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9 ambapo
Baba, Mama pamoja na watoto wao 3 ndiyo waliouawa.
Mushy
aliwataja waliofanyiwa unyama huo kuwa George Charles (30) ambaye ni
Baba wa familia, Siku John (23) Mama wa Familia na watoto wao ambao ni
Mchambi George (7) Tuma George (5) pamoja na Amos George (Miezi 9) wote
wasukuma wa kitongoji hicho.
Aidha
Kamanda Mushy alieleza chanzo kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu
(George) pamoja na Baba yake wa kambo ambaye alinunua kipande cha ardhi
alikokuwa akiishi marehemu.
Aliongeza
kuwa baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya msako na kuwakamata
watuhumiwa 3 ambao aliwataja kuwa ni Migata Lusalago (50) Jihelya Migata
(30), Solo Kengele (31) wote wasukuma wa kijiji cha Bugalama.
Kamanda
mushy alieleza kuwa waliokamatwa ni Baba wa kambo wa Marehemu pamoja na
watoto wake wawili ambao ilidaiwa kuwa wameweza kushiriki katika
kutenda tukio hilo la kinyama.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea
kufanyika ili kuwapata wahusika zaidi wa tukio hilo, ambapo aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano katika kudhibiti uhalifu ususani mauaji
yatokanayo na ukataji wa mapanga.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz


Post a Comment