Loading...

MTOTO WA MIAKA 5 ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHOMWA MOTO KWA MAFUTA YA PETROL

> JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HAPA CHINI UPATE NAFASI..

JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..



Mtoto Julias Makoye (5) mkazi wa mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga amenusurika kifo mara baada ya kuchomwa moto na jirani yao Edina Peter 20, kwa tuhuma ya kuiba simu na rimoti ya televisheni.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Kahamafm kuwa tukio hilo limetokea juzi ambapo Edina amefanya ukatili kwa mtoto Julias kwa kumwagia mafuta aina ya petrol mwili mzima na kisha kumchoma moto uliomsababishia majeraha mwilini.
Mwenyekiti wa mtaa wa mwendakulima kati Abrahamani Dulla, amefafanua kuwa mara baada ya Edina kutekeleza tukio hilo walimchukua mtoto Julias bila kuwapa taarifa wazazi wake na kumpeleka katika Zahanati ya Nyakato mjini Kahama.
Mama mzazi wa mtoto huyo Ndalo Manyanda amesema mwanaye alikuwa anacheza katika nyumba ya jirani na ghafla alipokea taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanaye amechomwa moto kwa tuhuma ya kuiba simu na rimoti ya televisheni.
Amesema hali ya mtoto wake inaendelea vizuri mara baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama huku akitoa rai kwa wasamaria wema kumsaidi fedha ili mwanaye apatiwe matibabu.
Jeshi la polisi wilayani kahama limetibitisha kutokea kwa tukio hilo na bado linaendelea kuwashikilia Chalya  Charles 30 na mkewe Edina aliyedaiwa kufanya tukio hilo kwaajili ya upelelezi wa tukio hilo.
>
JISHINDIE SAMSUNG GALAXY MPYA KABISA JAZA FOMU NA UTAPIGIWA SIMU PAPO HAPO BOFYA HAPO JUU,RUDIA KUBOFYA MPAKA UONE SIMU UNAPIGIWA =>

Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by Lovetzz

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WANAWAKE KWANZA | Modified By Zotekali WEB Exparts
Back To Top