Loading...

Waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura

> JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HAPA CHINI UPATE NAFASI..

JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote siku ya Jumapili.

Akizungumza katika mkutano wa vyama vya siasa na NEC mjini Dodoma jana, Ofisa Mwandamizi wa tume hiyo William Kitebi, alisema watu hao hawataruhusiwa hata kama majina na taarifa zao zipo kwenye Daftari la Wapiga Kura (BVR).

“Hakuna jinsi ya kuwasaidia watu waliopoteza kadi zao za kupigia kura ,”alisema Kitebi

Hata hivyo, Kitebi alisema kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye BVR  kuna baadhi ya mambo NEC wameyawekea utaratibu ili watu waweze kupiga kura.

Alisema watu ambao namba za kadi zinatofautiana na zile zilizopo kwenye BVR  lakini taarifa nyingine ni sahihi wataruhusiwa kupiga kura.

“Kuna wale ambao picha zao hazionekani kwenye daftari lakini kadi za kupiga kura wanazo, hawa wataruhusiwa kupiga kura,”alisema.

Kuhusu wale wapiga kura walioathiriwa na mipaka ya utawala, Kitebi alisema maamuzi ya tume kuwa watu hao watapiga kura kwenye kata walizopo.

“Kuna maeneo kulikuwa na mabadiliko ya mipaka ya kiutawala baada ya zoezi la uandikishaji kama Kishapu (Shinyanga) na Kaliuwa (Tabora), wao wataruhusiwa kupiga kura kwenye maeneo yao mapya,”alisema.

Kwa upande wa wapiga kura ambao wanakadi za kupigia kura lakini hawaonekani kwenye BVR, Kitebi alisema hao wamewekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura.

“Kama kule Mbarali (Mkoa wa Mbeya), kuna watu kama 6,000 ambao hawaonekani katika daftari lakini wanakadi na fomu zao zimejazwa na kuwasilishwa tume  hawa wanaruhusiwa kupiga kura,”alisema.
>
JISHINDIE SAMSUNG GALAXY MPYA KABISA JAZA FOMU NA UTAPIGIWA SIMU PAPO HAPO BOFYA HAPO JUU,RUDIA KUBOFYA MPAKA UONE SIMU UNAPIGIWA =>

Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by Lovetzz

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WANAWAKE KWANZA | Modified By Zotekali WEB Exparts
Back To Top