JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mtwara
Ufundi mkoani Mtwara, Tawfiq Hamisi (17), amefariki dunia baada ya
kukatwa na kiwembe katika mkono wake wa kulia na mwanafunzi mwenzake
Issac Yohana (16). Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, amesema kabla ya kifo hicho kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambaye ni Isaac anayedaiwa kuficha kiatu cha mwenzie ambapo baada ya mzozano akaamua kumkata na kiwembe mwenzie chini ya bega lake la kulia.
Ameongeza kuwa marehemu ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga huku mtuhumiwa ni mwenyeji wa wiayani Newala mkoani Mtwara, na kwamba taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka kwao zinafanywa na uongozi wa shule, huku mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Ligula, Dkt. Mdoe Mhuza, amethibitisha kupokelewa kwa mwili wa marehemu majira ya saa 11 alfajiri na kudai kuwa bado uchunguzi zaidi unaendelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanzo cha kifo chake.
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz


Post a Comment