JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Je penzi la kweli lipo ?
Hilo ndilo swali linaloulizwa sana katika mitandao nchini China.
Hii ni baada ya raia mmoja kutoka
Uholanzi kusafiri maelfu ya kilomita ili kukutana na mpenziwe raia wa
uchina ambaye walikutana kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo mpenziwe hakujitokeza hata baada ya kusubiri katika uwanja wa ndege kwa siku 10!
Amini usiamini alimsubiri kwa siku 10!
Alexander Pieter Cirk, 41, alifunga
safari hadi jimbo la Hunan kukutana na mpenziwe mwanamke kutoka Uchina
ambaye anafahamika kwa jina Zhang.

bi Zhang mwenye umri wa miaka 26 anasema alidhania kuwa ulikuwa ni mzaha tu
Na baada ya kumsubiri kwa siku kumi
katika uwanja wa ndege wa Changsha hakujitokeza ,,Cirk alienda kufanya
subira na mwishowe akalazimika kulazwa hospitalini kwa uchovu wa mwili
na roho.
Cirk ameviambia vyombo vya habari kuwa
walikutana na bi Zhang mwenye umri wa miaka 26 miezi miwili iliyopita na
penzi lao likachipuka.
Hata hivyo alipofika China akagundua kuwa wanawake wengi nchini humo wanafanana, na akashindwa kumpata Zhang kwa simu.
Ripoti hiyo ilipopeperushwa kwenye
runinga ya taifa , bi Zhang alijitokeza na kuwaamnbia Wachina kuwa
alidhania kuwa ni utani tu kama vile maisha ya mjini kwa wanawake wengi
ambao huambiwa kuwa wanapendwa.
''Ni kweli kuwa tulikuwa tunapendana lakini nilianza kumshuku huenda alikuwa ananichezea shere''
Alinitumia picha za tiketi ya ndege na hakunipigia simu baada ya hapo''
Kwa hivyo nikapuuza nikijua kuwa ni mzaha tu''bi Zhang aliiambia Hunan TV.

Alexander Pieter Cirk alilazwa hospitalini baada ya kuzimia
Zhang alisema kuwa ule wakati alipokuwa akimtarajia ,yeye alikuwa amefanyiwa upasuaji katika mji mwengine wa mbali.
Hangeweza kumpokea katika uwanja wa ndege.
katika mitandao ya kijamii tukio hilo limewaacha wengi wasijue iwapo ilikuwa ni penzi la kweli ama ni ujinga wa kuzaliwa.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz


Post a Comment