JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Askofu mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Rev. Josephat Gwajima
ametoa Onyo kali kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM
(taifa), bwana Abdallah Bulembo kwa kulitaja jina lake katika
mkutano wa kampeni za CCM huko Singida.
Onyo hilo limetolewa jana na Askofu Gwajima mbele ya waumini
wake huku akimtahadharisha Bulembo kuwa iwapo ataendelea, basi na
yeye ataibuka kutoka mafichoni ili kujibu mashambulizi.
"Nakuonya Bulembo, uache kunitaja kwenye mikutano yenu ya
kampeni.Ukiendelea kunitaja, nitapanda helkopta nikufuate huko huko
ili nijibu mapigo. Sitakujibu peke yako, ntawajibu na
waliokutuma.
"Nawatuma watu wa CCM mliopo kanisani kwangu mmwambie Bulembo aniache. Nikimjibu atasikitika.
"Nikiwajibu, utatoka moshi na hawatafungua macho. Ntawajibu wote na waliomtuma hadi nchi itatikisika."-Gwajima
Akiwa mkoani Singida kwenye mikutano ya kampeni za mgombea urais
wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, Bulembo anadaiwa kumtuhumu
Gwajima kwa kuandaa machafuko ili kuharibu amani ya nchi.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment