Loading...

TANZIA: MSANII WA NYIMBO ZA ASILI "NYANDA MADIRISHA" AFARIKI AKIJIANDAA KUFANYA SHOW HUKO SIMIYU..

> JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HAPA CHINI UPATE NAFASI..

JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..

 Wananchi wakishangaa mwili wa marehemu Nyanda Madirisha
 Pikipiki iliyoondoa uhai wa msanii Nyanda Madirisha


Gari la Msanii Nyanda Madirisha alilokuwa anatumia kufanyia show zake enzi za uhai wake.


Msanii wa nyimbo za asili kutoka Kahama mkoani Shinyanga maarufu kwa jina la Nyanda Madirisha amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki mkoani Simiyu alipokwenda kufanya show zake.

Wanawakekwanza.blogspot imeambiwa kuwa Msanii maarufu Nyanda Madirisha  amefariki  dunia leo Jumamosi Agosti 06,2016 mchana wakati akitoka kununua mafuta ya petrol kwa ajili ya jenereta analotumia kufanyia show zake kwenye gari lake  ambapo alitakiwa kufanya show siku ya Jumapili Agosti 07, 2016 katika eneo la Shinyanga Mwenge katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
“Alikuwa anatoka Lalago kuchukua mafuta ya petrol sasa wakati anatoka kuchukua mafuta hayo pikipiki ikamshinda na kumwangusha katika eneo la Mision ya Gula ambapo kuna kona akafariki papo hapo..show ya mbele ya pikipiki imenyofoka na hatuelewi sijui ameikosa kosaje hiyo kona”,mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ameiambia Malunde1 blog.
“Huenda kifo chake kimesababishwa na ulevi kwa sababu amekutwa na chupa za bia na viroba,pengine kutokana na kulewa ndipo pikipiki ilimshinda na kusababisha kifo chake papo hapo”,aliongeza shuhuda mwingine wa tukio hilo.

Wanawakekwanza.blogspot inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki wakiwemo wapenzi wa nyimbo za asili kwa msiba huu.
Pumzika kwa amani Nyanda Madirisha.
>
JISHINDIE SAMSUNG GALAXY MPYA KABISA JAZA FOMU NA UTAPIGIWA SIMU PAPO HAPO BOFYA HAPO JUU,RUDIA KUBOFYA MPAKA UONE SIMU UNAPIGIWA =>

Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by Lovetzz

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WANAWAKE KWANZA | Modified By Zotekali WEB Exparts
Back To Top