JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Janeth Ruzangi
Bandari ya Dar es Salaam inaingia katika historia mpya nyingine leo wakati meli ndefu kuliko zote zilizowahi kufunga katika bandari hiyo itakapoingia.
Meli hiyo yenye urefu wa mita 255, inatarajiwa kutia nanga nchini
na kufunga gati kesho Kampuni ya Kuhudumia Makontena nchini (Ticts)
katika Bandari ya Dar es Salaam.
Meli hiyo inayojulikana kama Clemens Schulte, ina uwezo wa kubeba
makontena 5,466 na inamilikiwa na moja ya kampuni kubwa duniani ya meli
ya Maersk Line.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Janeth
Ruzangi, alisema kuwasili kwa meli hiyo kutoka bandari ya Laem Chabang
ya nchini Thailand, ni uthibitisho wa kuongezeka kwa kuaminika kwa
Bandari ya Dar es Salaam.
“Bandari yetu inazidi kuaminika zaidi kadiri siku zinavyokwenda
kutokana na kuimarishwa kwa huduma pamoja na ulinzi na usalama wa mali
za wateja,” alisema.
Mkurugenzi wa Maendeleo Ticts, Donald Talawa, alisema mara ya
mwisho kampuni hiyo kupokea meli kubwa ilikuwa Februari, 2014 ambapo
meli ya Msc Martina iliyokuwa na urefu wa mita 242, ilitia nanga katika
Bandari ya Dar es Salaam.
Wakati wa safari hiyo ya kwanza, inatarajiwa kwamba MV Clemens
Schulte, itashusha makontena 250 na kupakia mengine 1,300, alifafanua
Talawa.
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz


Post a Comment