JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake ya awamu ya tano haitakuwa na blablabla katika utendaji wa kazi na kuonya kuwa waziri atakayeshindwa kutelekeza majukumu yake, ataondolewa ili kupisha wenye uwezo.
Dk. Magufuli alitoa ahadi hiyo jana, wakati akijinadi kwa wananchi
wilayani Nkasi na Kalambo, mkoani Rukwa akiwa katika siku ya pili ili
achaguliwe kuwa rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka
huu.
Alisema Baraza lake la Mawaziri ni lazima liwe na tofauti kubwa kwani watakuwa watumishi wa watu na siyo mabosi wa watu.
Alisema waziri atakayeteuliwa katika serikali hiyo, atampima na
akiona hawezi kutumiza majukumu yake ipasayo kwa wananchi, lazima
aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na waziri mwingine mwenye kasi ya
kufanya kazi kama yake, vinginevyo atawafukuza kila mara.
Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi, alisema atafanya
hivyo kwa sababu wananchi wanataka matatizo yao yatatuliwe kwa wakati na
si kusubiri siku inayofuata.
“Baraza langu litakuwa la kutetea wanyonge, litafanya kazi za
wananchi, nachukia uzembe na nitaonyesha kwa vitendo,” alisema na
kuongeza kuwa serikali yake itahakikisha fedha zinapelekwa kwa wananchi
kutekeleza miradi ya maendeleo.
“Ifike mahali tunaadhimisha wiki ya maji na maji yapo, wiki ya
nyama na nyama zipo, wiki ya Ukimwi na dawa zipo na wiki ya maziwa na
maziwa yapo,” alisisitiza. Vilevile, aliwaonya watendaji wazembe akisema
hawana nafasi kwani mwendo wake utakuwa ni wa mchakamchaka na
hakutakuwa na mapumziko hadi maendeleo yawafikie wananchi. Mgombea huyo
aliahidi kuunda serikali isiyo na kero kwa wananchi wa ngazi zote,
wakiwamo wa kipato cha chini, na itakuwa mkombozi kwa mamalishe na
waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kuwa itahakikisha zinafikia
mwisho.
NEEMA KWA MADAKTARI
Kwa upande mwingine, Dk. Magufuli aliahidi kuboresha mishahara na
maslahi mengine kwa madaktari na wauguzi ili kudhibiti wizi wa dawa za
serikali na kuziuza kwa wagonjwa kwenye maduka yao na kusababisha
hospitali, vituo vya afya na zahanati kukosa dawa.
“Tunataka hospitali na zahanati zetu ziwe na dawa za kutosha, mwananchi apate huduma nzuri,” alisema.
Kadhalika, alisema serikali yake ina mpango wa kujenga zahanati
katika vijiji vyote, vituo vya afya kwenye kata, hospitali wilayani na
hospitali za rufaa mikoani ili kusogeza huduma za matibabu karibu na
wananchi na kuwaondolea kero ya kusafiri kufuata huduma hiyo mbali na
makazi yao.
ELIMU BURE
Dk. Magufuli aliahidi kuwa akiingia madarakani baada ya
kuchaguliwa, kitaumbele cha kwanza kitakuwa ni kutoa elimu bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne huku akiwataka Watanzania
kuzaliana kwa wingi kwa kuwa serikali itabeba jukumu la kusomesha watoto
wao.
Alisema fedha za kutekeleza hilo zipo kwa kuwa atakuwa amedhibiti
mafisadi na wezi wa mali za umma.Mgombeaurais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli,
amesema serikali yake ya awamu ya tano haitakuwa na blablabla katika
utendaji wa kazi na kuonya kuwa waziri atakayeshindwa kutelekeza
majukumu yake, ataondolewa ili kupisha wenye uwezo.
Dk. Magufuli alitoa ahadi hiyo jana, wakati akijinadi kwa wananchi
wilayani Nkasi na Kalambo, mkoani Rukwa akiwa katika siku ya pili ili
achaguliwe kuwa rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka
huu.
Alisema Baraza lake la Mawaziri ni lazima liwe na tofauti kubwa kwani watakuwa watumishi wa watu na siyo mabosi wa watu.
Alisema waziri atakayeteuliwa katika serikali hiyo, atampima na
akiona hawezi kutumiza majukumu yake ipasayo kwa wananchi, lazima
aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na waziri mwingine mwenye kasi ya
kufanya kazi kama yake, vinginevyo atawafukuza kila mara.
Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi, alisema atafanya
hivyo kwa sababu wananchi wanataka matatizo yao yatatuliwe kwa wakati na
si kusubiri siku inayofuata.
“Baraza langu litakuwa la kutetea wanyonge, litafanya kazi za
wananchi, nachukia uzembe na nitaonyesha kwa vitendo,” alisema na
kuongeza kuwa serikali yake itahakikisha fedha zinapelekwa kwa wananchi
kutekeleza miradi ya maendeleo.
“Ifike mahali tunaadhimisha wiki ya maji na maji yapo, wiki ya
nyama na nyama zipo, wiki ya Ukimwi na dawa zipo na wiki ya maziwa na
maziwa yapo,” alisisitiza. Vilevile, aliwaonya watendaji wazembe akisema
hawana nafasi kwani mwendo wake utakuwa ni wa mchakamchaka na
hakutakuwa na mapumziko hadi maendeleo yawafikie wananchi. Mgombea huyo
aliahidi kuunda serikali isiyo na kero kwa wananchi wa ngazi zote,
wakiwamo wa kipato cha chini, na itakuwa mkombozi kwa mamalishe na
waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kuwa itahakikisha zinafikia
mwisho.
NEEMA KWA MADAKTARI
Kwa upande mwingine, Dk. Magufuli aliahidi kuboresha mishahara na
maslahi mengine kwa madaktari na wauguzi ili kudhibiti wizi wa dawa za
serikali na kuziuza kwa wagonjwa kwenye maduka yao na kusababisha
hospitali, vituo vya afya na zahanati kukosa dawa.
“Tunataka hospitali na zahanati zetu ziwe na dawa za kutosha, mwananchi apate huduma nzuri,” alisema.
Kadhalika, alisema serikali yake ina mpango wa kujenga zahanati
katika vijiji vyote, vituo vya afya kwenye kata, hospitali wilayani na
hospitali za rufaa mikoani ili kusogeza huduma za matibabu karibu na
wananchi na kuwaondolea kero ya kusafiri kufuata huduma hiyo mbali na
makazi yao.
ELIMU BURE
Dk. Magufuli aliahidi kuwa akiingia madarakani baada ya
kuchaguliwa, kitaumbele cha kwanza kitakuwa ni kutoa elimu bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne huku akiwataka Watanzania
kuzaliana kwa wingi kwa kuwa serikali itabeba jukumu la kusomesha watoto
wao.
Alisema fedha za kutekeleza hilo zipo kwa kuwa atakuwa amedhibiti mafisadi na wezi wa mali za umma.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz

Post a Comment