JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mmiliki wa klabu ya Chelsea ya Uingereza raia wa Urusi Roman Abramovich
tumezoea kuona akifukuza makocha kwa haraka zaidi endapo tu mwenendo wa
timu yake utakuwa sio mzuri kwa kipindi kifupi, tabia ya tajiri huyo wa
Kirusi imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa kutimuliwa kazi kwa Jose Mourinho kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya
Wakati wengi wakiwa wanahisi kuwa huenda Jose Mourinho atafukuzwa kazi muda wowote kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa Southampton, mchana wa October 5 tovuti ya Chelsea
iliandika ujumbe ambao unatajwa kuwa utaongeza kujiamini kwa timu na
kocha, kwani katika kipindi kigumu kama hiki, huwa ni kawaida kwa kocha
na wachezaji kupoteza hali ya kujiamini.
“Klabu
inaweka wazi kuwa Jose Mourinho ataendelea kuungwa mkono na klabu kama
kawaida, licha ya kuwa Jose Mourinho alisema timu imekuwa haina matokeo
mazuri na inahitaji kuimarika, hivyo tunaamini tuna kocha mzuri msimu
huu na anaweza kuleta mafanikio”>>> Chelsea
Chelsea ina wakati mgumu katika msimu huu kwani imecheza mechi nane, imeshinda mbili, sare mbili na kufungwa michezo minne, kwa sasa Chelsea ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza. Jose Mourinho aliwahi kuwa kocha wa Chelsea katika kipindi cha mwaka 2004 hadi 2007 na kufukuzwa kazi na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich, kabla ya kurejea kwa mara ya pili mwaka 2013.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment