Loading...

Lowassa Ampongeza Kingunge Kwa Kujiondoa CCM.....Atangaza Neema Kwa Wenyeviti Serikali za Mitaa

> JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HAPA CHINI UPATE NAFASI..

JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..


MGOMBEA Urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendele (Chadema), Edward Lowassa, amesema akiingia madarakani, Serikali yake itawalipa posho wenyeviti wa Serikali za vijiji, wenyeviti wa mitaa na wenyeviti wa vitongoji kwa kuwa wanafanya kazi kubwa.

Lowassa ambaye jana alifanya mikutano mitano ya kampeni   Magugu, Dongobesh, Bashinet na Haidom, aliyasema hayo akiwa kwenye mkutano wa kampeni Makondeko, Kateshi, wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.

“Serikali yangu ikiingia madarakani  wenyeviti wa vijiji, vitongoji, mitaa tutawalipa posho. Lazima tugawane keki ya nchi kwa sababu hawa wanafanya kazi kubwa, lazima walipwe,” alisema Lowassa.

Lowassa anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alimpongeza mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru kwa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nampongeza Kingunge kwa kukubali mabadiliko,” alisema Lowassa.

Akiwa kwenye mji mdogo wa Magugu, Lowassa alisema Serikali yake itajenga hospitali mpya za kisasa zenye vifaa vyote na wataalamu.

Kuhusu elimu alisema wapo watu wanaokejeli sera ya kutoa elimu bure kuanzia shule za watoto wadogo mpaka chuo kikuu wakihoji atapata wapi  fedha.

Kama nchi ina   gesi, madini na inaweza kununua mashangingi haiwezi kushindwa kutoa elimu bure, alisema.

“Nagombea ili nipambane na umasikini, ninaamini hakuna urithi utakaoweza kumpa mtoto wako kama siyo elimu  ndiyo maana nasema kipaumbele changu cha kwanza ni elimu, cha pili ni elimu na cha tatu ni elimu,” alisema.

Baada ya elimu, alisema atahakikisha anaboresha kilimo ikiwa ni pamoja na kutafuta soko la uhakika kwa bidhaa za wakulima na kuwaruhusu kuuza mazao yao popote penye soko.

Naye  Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, akiwa   Magugu, alisema kuna njama chafu zinaendeshwa za kuwaeleza wananchi siku ya kupiga kura watakuta jina la Ukawa na siyo vyama vinavyounda umoja huo.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD.

“Kwenye karatasi ya kura hamtakuta jina la Ukawa, mtakuta majina ya vyama, rais mtampigia anatoka Chadema na wagombea wengine wako kwenye vyama husika,” alisema Sumaye.

Aliwataka  wananchi hao kuhakikisha wanawahi kwenye vituo vya kupigia kura ili wasikose fursa hiyo kutokana na njama za wapinzani wao wa siasa.
>
JISHINDIE SAMSUNG GALAXY MPYA KABISA JAZA FOMU NA UTAPIGIWA SIMU PAPO HAPO BOFYA HAPO JUU,RUDIA KUBOFYA MPAKA UONE SIMU UNAPIGIWA =>

Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by Lovetzz

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WANAWAKE KWANZA | Modified By Zotekali WEB Exparts
Back To Top