JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli, jana aliwaongoza
wanachama wa chama hicho kuupokea mwili wa Dtk. Abdallah Kigoda
aliyepoteza maisha nchini India, ambapo alieleza kuwa alimpa ushauri
katika kipindi kifupi kabla Mungu hajamchukua.
Akiongea na waandishi wa habari, Magufuli alieleza kuwa Marehemu Kigoda
alimshauri masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasaidia
wawekezaji na wafanyabiashara wazalendo.
Alisema
kifo cha Dkt.Kigoda ni pigo kubwa kwa Watanzania wote kwani alikuwa na
moyo wa kuwatumikia Watanzania ili wapate maendeleo.
"Nitamkumbuka
Dkt.Kigoda kwa mengi; ila nakumbuka alipokuwa Apollo nchini India
aliposikia naenda jimboni kwake aliomba ruhusa ya siku moja; akaja
tukaungana kule jimboni kwake ambapo nilimkabidhi ilani ya uchaguzi
kisha akarudi Apollo kuendelea na matibabu", alisema Dkt.Magufuli na kuongeza:
"Kabla
ya kupelekwa ICU (Chumba cha uangalizi maalumu) alinipigia simu na
kunipa ushauri jinsi ya kuwajali na kuwasaidia wafanyabiashara wa ndani;
hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwetu".
Ombeni Sefue
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema kifo cha
Dkt.Kigoda ni pigo kubwa kwa Serikali kwani ni Waziri ambaye amefanya
kazi kubwa ya kuwatumikia Watanzania.
"Kifo
chake ni pigo kubwa sana kwa Watanzania na Serikali kwa ujumla kwani ni
waziri ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu katika kuwatumikia
Watanzania," alisema Balozi Sefue.
Mwili
wa Dkt. Kigoda uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 9 na dakika 35 alasiri kwa
Ndege ya Shirika la Emirates.
Mwili huo ulipokewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya siasa.
Baadhi
ya viongozi walioshiriki kwenye mapokezi hayo ni mgombea urais kupitia
CCM, Dkt.John Magufuli,Spika wa Bunge, Anne Makinda pamoja na Waziri wa
Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe.
Mpekuzi blog
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment