JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema mgawo wa umeme kwa sasa hauzuiliki nchini kutokana na mabwawa yanayotumika kuzalisha nishati hiyo nchini kukumbwa na ukame.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa uzalishaji wa umeme wa maji kwenye mabwawa hayo
umeshuka hadi kufikia megawati 105 kutoka 561 kutokana na ukame
unaoendelea majira haya ya kiangazi.
Mramba
alisema hali hiyo imeilazimu Tanesco kutegemea kwa kiasi kikubwa umeme
unaozalishwa na mitambo ya mafuta na gesi asilia hasa ile ya Kinyerezi
I, ili kupunguza makali ya mgawo huo kwa kuwasha mtambo mmoja baada ya
mwingine hadi mwishoni mwa Oktoba.
Alisema hadi kufikia jana, mabwawa yote makubwa yalikuwa na maji kidogo hivyo kushusha uzalishaji wa umeme kwa asilimia 81. 3.
“Bwawa
la Mtera ambalo huzalisha megawati 80 kwa sasa halizalishi kwa kuwa
hakuna maji, Kidatu lenye kuzalisha hadi megawati 204 kwa sasa
linazalisha megawati 27 tu, Kihansi lenye uwezo wa juu wa kuzalisha
megawati 180 linazalisha megawati 51. 5,” alisema Mramba.
Alisema
hali kama hiyo ipo katika vyanzo vya maporomoko ya maji ya Pangani
ambako uzalishaji umeshuka kutoka megawati 68 hadi 17, mtambo wa Hale
kutoka 21 hadi 8, Bwawa la Nyumba ya Mungu kutoka 8 hadi 5. 5.
Mramba
alisema mgawo huo pia unatokana na kushuka kwa kiwango cha uzalishaji
gesi ya ya Songo Songo, ambako Kampuni ya Pan Africa inafanya ukarabati
wa visima baada ya kubaini uzalishaji ulikuwa ukishuka kutoka megawati
340 hadi 260.
“Wananchi wawe watulivu mgawo huu hauna siasa hata chembe bali ni masuala ya kiufundi tu,” alisema Mramba.
Hata
hivyo, alisema neema itaanza kuonekana leo kwa wakazi wa Dar es Salaam
ambao huenda makali ya mgawo wa umeme yakapungua baada ya mtambo mpya wa
megawati 35 kuwashwa jana kwa kutumia bomba jipya la gesi.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment