JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Mtayarishaji wa vipindi, Sospiter Jonas amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma Mjini akishtakiwa kwa matumizi mabaya ya mtandao.
Sospiter alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mussa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Emmanuel Bwile.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook ujumbe kuwa “Pinda utakuwa muhubiri wa injili tu.”
Mussa
aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa huyo alibandika picha ya John Maliga
kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika ujumbe huo, kitendo ambacho
ni kinyume cha kifungu namba 16 cha Sheria ya Mtandao ya Mwaka 2015.
Mlalamikaji katika shauri hilo la jinai namba 815/2015 litakalokuja tena mahakamani Oktoba 19, ni John Maliga.
Mshtakiwa yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja na bondi ya Sh1 milioni.
Kesi
hii imekuja baada ya wiki iliyopita, kijana mmoja, Benedict Ngonyani
(24) kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
akituhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange.
Kijana
huyo anatuhumiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook na WhatsApp
kuwa, Mwamunyange, amelazwa kwenye hospitali moja mjini Nairobi, Kenya
kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu.
Mpekuzi blog
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment