JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
WAPENZI wanagombana, ndoa
zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye msoto kwa sababu ya ubinafsi.
Tunazungumza mengi lakini ukweli ni kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa
kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri kila kona.
UBINAFSI UNA
MATAWI MENGI.
Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa
binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa
kulinda penzi la mwenzake.
Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu.
Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe.
Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu
alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma.
Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo
sivyo.
Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi.
Umeingiwa na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili wako, kwa
hiyo unaweza kukitumia bila kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni tabia mbaya mno.
Kabla ya kusaliti, fikiria
Kama inauma, ni kwa nini umtende mwenzako? Je, umemuona yeye
hana moyo? Anza leo kukemea ubinafsi. Popote pale utakapoona unachukua nafasi,
upinge kwa sababu ni adui mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote usiseme “nipo”,
sema “tupo”.
Unapozunguka, usiwaze “upo”, unatakiwa kuwaza “mpo”. Hii
itakusaidia kulinda siti ya mwenzako kila utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya
mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa mkopo. Kama ilivyo kwenye soka, wachezaji
huchezea timu nyingine kwa mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa yalivyo.
Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini anavyojieleza anatoa
picha kwa muulizaji kuona kwamba aliyepo si muhimu sana. Hii husababisha muulizaji aombe kukaa na baadaye hukaribishwa. Wengi walikaribishwa kwa mkopo, mwisho wakawa wamiliki wa jumla.
picha kwa muulizaji kuona kwamba aliyepo si muhimu sana. Hii husababisha muulizaji aombe kukaa na baadaye hukaribishwa. Wengi walikaribishwa kwa mkopo, mwisho wakawa wamiliki wa jumla.
Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba anaweza kukaa, wakati unajua
siti ina mmiliki wake halali? Kwa porojo za kitoto, eti mnaambiana mfanye siri.
Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na mwenzako naye kagawa siti yako kwa
mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.
Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali unatakiwa uache
ubinafsi. Haliitwi penzi bila kuwepo watu wawili. Lazima uhakikishe unalinda la mwenzako ili na lako lilindwe. Somo la mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie mwingine.
ubinafsi. Haliitwi penzi bila kuwepo watu wawili. Lazima uhakikishe unalinda la mwenzako ili na lako lilindwe. Somo la mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie mwingine.
Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa wananchi pale kiongozi mwenye
dhamana kiserikali anaposhindwa kutimiza majukumu yake na kuamua kushughulikia shida
zake binafsi, huku akitumia rasilimali za umma, ni kirusi hatari kila upande.
Baba anapoamua kufuja fedha wakati anajifahamu anayo familia
inayomtegemea, huo ni ubinafsi. Anafikiria kutumbua yeye binafsi, wakati
anatakiwa kujenga msingi wa familia. Anashindwa kujua kwamba fedha anazotafuta
si zake peke yake.
Kama anaona anatakiwa kutumia fedha zake peke yake, basi hapaswi
kujipa mzigo wa kumiliki familia. Mtu anapokuwa baba au mama, uamuzi wake
unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi.
Kumaliza mshahara kwenye kumbi za starehe ni ukatili kwa
familia hususan mtoto ambaye hautakavyoumia pindi utakaposalitiwa.
Usijidanganye kwamba unajimiliki mwenyewe. Wewe
unamilikiwa na familia yako, kwa hiyo una deni na wajibu mkubwa kwa wale
wanaohusika. Kabla ya kwenda nyumba ya kulala wageni na huyo unayemtamani,
fikiria kwamba unamilikiwa.
Baba au mama, anapokwenda hoteli na mpenzi wa nje. Akakubali
kuvua nguo na kufanya mapenzi. Ajitambue kuwa anachezea maisha ya watu wengine.
Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe na afya njema ili wanaokumiliki waendelee
kupata huduma yako.
Unafahamu kwamba mapenzi yanaua.
Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa mtulivu nyumbani, unaiba
muda wa familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako ila ni za familia. Unaweza
kupata picha kwamba viungo ni vyako lakini penzi si lako. Ukilitoa ni wizi, ni
dhuluma iliyopitiliza.
ZAIDI
kukuomba umlete duniani
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz


Post a Comment