JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Serikali imesema zaidi ya Sh. bilioni 230 zimepotea katika kipindi cha mwaka uliopita kutokana na ajali za barabarani nchi nzima.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina ya madereva wa magari
makubwa, mabasi ya masafa marefu na daladala jijini Mwanza juzi, Mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga (pichani), alisema kiasi cha Sh.
bilioni 230 zilipotea katika ajali zilizotokea kipindi hicho licha ya
baadhi ya ajali hizo zingeweza kuepukika.
Katika semina hiyo ya kuwaelimisha madereva juu ya makosa ya
kibinadamu yanavyochangia kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani,
Konisaga alisema uzembe, ulevi, uchakavu wa barabara, ubovu wa magari ni
miongoni mwa sababu hizo.
“Katika kipindi cha mwaka jana pekee Sh. bilioni 230 zilipotea
kutokana na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani ambazo nyingi
zimesababishwa na makosa ya binadamu,” alisema.
Awali akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Usalama Barabarani
na Mazingira wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu
(Sumatra), Geofrey Silanda, alisema tafiti mbalimbali zilizofanywa
nchini zinaonyesha asilimia 75 za ajali za barabarani zinatokana na
makosa ya kibinadamu.
“Lakini pia asilimia 50 ya makosa hayo ya barabarani yanayohusiana
na mambo ya kibinadamu yanafanywa na madereva,” alisema Silanda.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mabasi
Mkoani Mwanza (Uwamata), Shabani Wandiba, aliitupia lawama serikali kuwa
ndiyo inayochangia kwa kiasi kikubwa kusababisha ajali za barabarani
kutokana na kupanga muda wa magari kusafiri bila ya kuangalia umbali.
“Ratiba inapangwa bila kuangalia umbali, mwendo kulingana na alama
za barabarani, mfano mwendo wa kilomita 80, 50, 20 kwa saa pamoja na
muda wa chakula yote hayo ni miongoni mwa vyanzo vya ajali,” alisema
Wandiba.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza,
Mrakibu wa Polisi Mohamed Likwata, alisema ajali nyingi zinasababishwa
na madereva ambao wanashindwa kufuata sheria na alama za usalama
barabarani kikamilifu.
Kuhusu muda, kamanda huyo alisema atashauriana na Sumatra kuangalia
muda wa chakula wa dakika 10 ili uweze kuongezwa kutokana na mabasi
yenye uwezo wa kuchukua abiria 60 kutoweza kutimiza sheria hiyo ambayo
inawabana madereva.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz



Post a Comment