JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..
Akizungumza
kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni zake kwa Mkoa wa Arusha, mgombea
huyo alisema Dk Magufuli ni mtendaji ndiyo maana anasisitiza kujenga
madaraja na barabara kila anakokwenda.
“Kazi
ya rais si kujenga barabara, sasa kwa kuwa yeye yuko vizuri katika
suala la ujenzi nichagueni niwe rais wenu ili nije kumchagua aendelee
kujenga barabara, kazi anayoifanya kwa ufanisi,” alisisitiza.
Awali,
katika mikutano aliyofanya katika majimbo ya Arumeru Magharibi, Arumeru
Mashariki na Arusha Mjini, mgombea huyo alisema Serikali yake ina sera
mahsusi kwa ajili ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa nchini ukiwa umezungukwa na rasilimali mbalimbali.
Alisema mkoa huo pekee wenye madini ya Tanzanite nchini na duniani kwa ujumla, pia una mbuga mbalimbali za wanyama.
Kwa upande wa kilimo, alisema mazao kama kahawa, maua, vitunguu maji na mbogamboga ni vipaumbele vyake.
“Tunataka
Watanzania wajiwekee akiba ili tutunishe mifuko ya hifadhi ya jamii.
Katika utawala wetu tunataka watu milioni tano waingie kwenye mifuko ya
hifadhi ya jamii kwa kipindi cha mwezi mmoja,” alisema na kuongeza:
“Ukiweka Sh10,000 Serikali itakuongezea Sh20,000, hivyo kila mwezi utakuwa na uhakika wa kuingiza Sh30,000,” alisema.
Alisema mfumo wa maisha ya Watanzania unahitaji kufanyiwa mabadiliko na wao ndio wanaopaswa kusimamia suala hilo.
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment