JE WEWE UNA ELIMU YA KIDATO CHA NNE ?PATA AJIRA NA UJIONGEZEE KIPATO HADI LAKI 8 KWA MWEZI WAHI NAFASI NI CHACHE BOFYA HIYO PICHA HAPO JUU UPATE NAFASI.. ..LIKE PAGE !..

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakazi wa jiji la Mwanza
na vitongoji vyake katika uwanja wa Furahisha mapema jana kwenye mkutano
wa hadhara wa Kampeni za CCM zilizohudhuriwa na Maelfu ya watu.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Misungwi mkoani
Mwanza waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM
uliofanyika wilayani humo wakati alipoomba kura za ndiyo kwa wananchi
ili wamchague na kuwa rais wa Tanzania katika uchaguzi wa Rais, Wabunge
na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini kote
ukishirikisha vyama vingi vya siasa
Dk. John Pombe Magufuli amefanya
mikutano katika miji ya Mugu, Ngudu katika jimbo la Sumve na mji wa
Misungwi katika wilaya ya Misungwi mkutano uliohudhuriwa na wananchi
wengi huku wakikatiza hotuba ya mgombea huyo wakati walipokuwa wakiimba
nyimbo Rais, Rais, Ameongeza kwamba atahakikisha anaboresha kilimo cha
Pamba na kuweka bei nzuri ya Pamba huku akiondoa ushuru usiokuwa wa
lazima kwenye mazao ili wakulima wa zao hilo waweze kunufaika na kilimo
chao.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MISUNGWI)
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi
wa mji wa katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika mjini Misungwi
mkoani Mwanza leo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa Kampeni za CCM uliofanyika mjini Misungwi mkoani Mwanza leo.
Baadhi ya wagombea udiwani wa jimbo la Misungwi wakiwa katika mkutano huo.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaimbisha wakazi wa mji wa Misungwi
mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa kampenzi za CCM.
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya
CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Alhaji Abdallah Bulembo
akiwahutubia wananchi wa mji wa Misungwi kabla ya kumkaribisha Mgombea
urais Dk. John Pombe Magufuli awahutunie wananchi.
Wasanii wa Teamstuka wakishuka jukwaani mara baada ya kufanya vitu vyao jukwaani kwa kumpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
Mwigizaji Kajala Masanja akishuka jukwaani na wenzake.
Waigizaji hao wakisalimiana na Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kupiga debe katika mkutano huo.
Wakifanya vitu vyao jukwaani.
Msanii Malaika akitumbuiza katika mkutano huo.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa jukwaa kuu pamoja na viongozi
mbalimbali wakati wa mkutano huo kutoka kulia ni Katibu wa CCM Mwanza
Miraji Mtaturu, Alhaji Abdallah Bulembo, Anthony Dialo mwenyekiti wa CCM
Mwanza na kushoto ni Mh. Charles Kitwanga mgombea ubunge jimbo la
Misungwi.
Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu akihutubia mkutano wa kampeni za CCM mjini Misungwi.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Ngudu jimbo la Sumve mkoani Mwanza.
Baadhi ya wananchi
wakimshangilia Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe
Magufuli wakati akihutubia wakazi wa mji wa Ngudu mkoani Mwanza
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wagombea ubunge wa majimbo ya
Kwimba na Sumve mkoani Mwanza kulia ni Richard Ndasa na Mansoor
Shanif katikati wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji wa
Ngudu wilayani Kwimba.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliomsimamisha
katika mji wa Kisesa ili asalimiane nao.
Mgombea ubunge wa jimbo la Magu
Kiswaga Boniventura Destery akiwaomba kura wananchi wa mji wa Magu ili
wampigie Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mji wa Magu leo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Magesa
Mulongo kushoto na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga
wakifutrahia jambo wakati walipokuwa wakizungumza.
Huyu mama aliamua ktoka na taulo ili mradi aweze kumuona Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mabatini wakati
aliposimamishwa ili kuwasalimia.
wananchi wa Mabatini jijini Mwanza wakimshangilia Dk. John Pombe Magufuli.
>
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by Lovetzz
Post a Comment